Ijumaa 27 Machi 2026 - 06:00
Hatuitetei Iran, bali zaidi ya hapo, tuko kwenye mstari mmoja na Iran

Hawza/ Mahmoud Arıkan, Kiongozi wa Chama cha Saadet cha Uturuki, katika hotuba yake, huku akikosoa mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran na maendeleo ya hivi karibuni katika Mashariki ya Kati, amesisitiza kwamba; suala la Iran sio la kidini au la kihistoria, bali ni suala la kijiografia (geopolitical) na kimkakati, na Uturuki na Iran kwa pamoja hazina budi kusimama kwenye mstari mmoja kukabiliana na vitisho vya pamoja.

Kwa mujibu wa taarifa ya Huduma Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Mahmoud Arıkan, Kiongozi Mkuu wa Chama cha Saadet, katika hotuba yake, alitoa tathmini ya maendeleo ndani ya Mashariki ya Kati.

Akirejelea mabadiliki ya kikanda, alisema: "Kwa bahati mbaya, pia tumepitia sikukuu hii kwa wasiwasi na ghadhabu kutokana na shule zilizoshambuliwa nchini Iran; pia milipuko dhidi ya Lebanon na hali ya kusikitisha ya Msikiti wa Al-Aqsa. Kufungwa kwa Msikiti wa Al-Aqsa, mojawapo ya sehemu takatifu zaidi za ibada katika ulimwengu wa Kiislamu, kwa ajili ya ibada katika mwezi wa Ramadhani, mwezi mtakatifu zaidi wa Kiislamu, ni hali isiyokubalika."

Arıkan, akisema kuwa kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi ya ibada, swala za Eid hazikufanyika katika Msikiti wa Al-Aqsa, aliongeza: "Beirut ilichomwa na kuharibiwa na mabomu ndani ya mwezi wa Ramadhani. Watoto waliuawa nchini Iran, na ubinadamu ulikufa katika dhamiri. Bila shaka, yote haya yana sababu moja tu; sio mpango wa nyuklia, sio makombora ya balestiki, sio haki za wanawake, wala kitu kingine chochote. Marekani na Israel wanataka kuwafanya watu wa eneo hili kuwa 'watumwa wao' kwa maana halisi."

Arıkan, katika tathmini yake ya mashambulizi dhidi ya Iran, alisema, "Hatuitetei Iran; tuko kwenye mstari mmoja na Iran," na kuongeza: "Katika mradi mkuu wa Marekani wa Mashariki ya Kati, hakuna tofauti kati ya Uturuki na Iran. Katika lengo la 'ardhi ya ahadi' ya Israel, hakuna tofauti kati ya Uturuki na Iran. Mwishowe, kama Iran ilivyo lengo machoni mwa Wazayuni, vivyo hivyo na Uturuki ni lengo. Kwa hivyo, Uturuki na Iran hazina budi kusimama kwenye mstari mmoja. Suala la Iran leo, sio suala la 'kidini' ambalo baadhi ya duru zinasisitiza kulichambua kupitia mtazamo wa tofauti za kidini. Pia, sio suala la 'kihistoria' ambalo linapaswa kuchambuliwa kulingana na tofauti za kihistoria kwa mujibu wa baadhi ya mikondo. Leo, suala hili ni la kijiografia (geopolitical), kiuchumi, na la idadi ya watu. Uturuki, katika nyanja hizi tatu zote, inakabiliwa na athari mbaya za vita nchini Iran. Amani ya ndani, utulivu, na usalama wa majirani zetu ni wa thamani kwa mustakabali wa eneo letu."

Arıkan pia alijibu matamshi ya Donald Trump, Rais wa Marekani, kuhusu Iran, akisema: "Amesema ameahirisha mashambulizi dhidi ya vituo vya nishati vya Iran kwa siku tano. Subiri dakika moja, wewe ni nani? Unampa nani na kwa nini muda? Unampa nani? Ewe Trump! Hizi ni siku zako nzuri tu. Hivi karibuni hata shimo la kukimbilia hutolipata. Maneno haya yako sio kitu zaidi ya jaribio la kununua muda, linalotokana na kukata tamaa kunakotokana na kukwama kwenye kona. Mahesabu ya Washington hayakufua dafu mjini Tehran na sasa mnajaribu kuyaficha. Vituo vyenu katika eneo viliharibiwa, ngao zenu za chuma zikageuka kuwa vichungi, na mmeghariki katika maji ya Hormuz."

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha